Sunday, April 17, 2011

Tegemeza Viwawa Jimbo kuu la Dar es salaam

Viwawa Upanga waongoza katika makusanyo ya Tegemeza Viwawa Jimbo kuu la Dar es salaam....

Leo ilikua ni siku ya mwisho kwa Maparokia yote walio chukua kadi za Tegemeza Viwawa Jimbo kuu la Dar es salaam Kuwasilisha kadi na Michango yao, katika Misa ya Matawi Iliyo adhimishwa na Mwasham Baba Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es salaam baba Libena katika Ukumbi wa Don Bosco - Upanga ambapo Viwawa parokia Ya Mt Immaculata Upanga walishika nafasi ya kwanza kwa Kuwasilisha jumla ya Sh 433,000/= fedha taslimu, Nafasi ya pili ilikua ni Parokia ya Mkuza kwa jumla ya Sh 300,000/=, Nafasi ya tatu Parokia ya Chang`ombe Sh 245,000/= na nafasi ya nne parokia ya Magomeni kwa jumla ya Sh 206,000/=....Fedha hizi zilichangwa na Vijana katika Jumuiya zao na Wakristu wengine wenye mapenzi mema..Tunazishukuru Jumuiya zote za Parokia ya Upanga, Baba Paroko Fr. Francis Borri, Baba Paroko Msaidizi Fr. Silvanos, Masista wa Parokia, Viongozi wote wa Kanda na Wanaparokia wote kwa Ujumla kwani bila ninyi Viwawa Jimbo Kuu la Dar es salaam Lisinge weza kupata Fedha Hizi..Tunasema Asanteni.